MALEZI NA ULINZI WA MTOTO

Umakini wa wazazi katika malezi ya mtoto ni muhimu kwa afya bora na mafanikio ya mtoto.

Obedi (jina la kubuni) ni mtoto mwenye umri wa miaka 9 na mwanafunzi wa darasa la tatu anaeishi na wazazi wake katika moja ya kata ndani ya wilaya ya Morogoro Mjini. Obedi katika Maisha ya kila siku ya kwenda shule asubuhi nakurudi nyumbani jioni alikutana na Mzee Mapambano (jina la kubuni) ambae alisadikika kuwa mganga wa kienyeji, mzee Mapambano alimzoea mtoto Obedi na kuanza kumkaribisha kwake kama mjukuu wake.

Obedi alikua akitembea na Rafiki zake nane wote wa kiume kama yeye hivyo wote walikua wakienda kumtembelea mzee Mapambano. Mzee huyo hakuwa na maadili kwani alianza kuwataka watoto hao kimapenzi kwa nguvu hata kwa kutumia vitisho, hii ilipelekea watoto hao kukubali matakwa ya mzee huyo na kuanza kuingiliwa na mzee huyo kinyume na maumbile (kulawitiwa). Watoto walilazimika kuripot kwa mzee huyo kila siku baada ya kutoka shule bila kukosa kwasababu ukikosa ulikua ukiadhibiwa kwa viboko vingi. Watoto hao waliogopa kusema kwa wazazi wao lakin pia hata kwa walimu wao. Kitendo hicho kilidumu kwa muda wa miezi sita mfululizo.

Siku moja Obedi alitoka shule akiwa na mwendo usio wa kawaida mama ake ikabidi amuulize mbona hautembei vizuri nini shida? Obedi kwa woga alijibu nimeumia mguu, mama yake ilibidi amuangalie mguuni lakin hakukuwa na jeraha lolote mguuni, mama ake akaona ni vyema kumuogesha mwanae kwa siku hiyo kwasababu alionekana hayuko sawa. Mama Obedi akiwa anamuogesha mwanae aligundua mwanae hayuko sawa katika sehemu zake za siri na alitambua mtoto anafanyiwa kitendo kibaya, mtoto aliulizwa na mama yake huwa unafanya nini mbona upo katika hali hii? Obedi alilazimika kumwambia mama ake ukweli wa mambo.

Siku iliyofata mama Obedi na mtoto wake waliripoti tukio kwenye ofisi ya kata, mtoto alihojiwa na kuelezea tukio lote hata kuwataja na marafiki zake ambao huwa wanaenda wote kwa mzee Mapambano. Afisa mtendaji wa kata ilibidi awaite watoto wote na wazazi wao kwa ushahidi zaidi, watoto walikiri uwepo wa tukio hilo, hivyo ilibidi watoto wote tisa wapelekwe hosptali kwa vipimo zaidi, majibu ya hosptali yalithibitisha kulawitiwa kwa watoto hao lakini pia yalithibitisha kuwa wamepata maambukiz ya virusi vya ukimwi kwa watoto wote tisa. Hatua za kisheria ilibidi zifuatwe kwa kuripoti kesi hiyo kituo kikubwa cha polisi Morogoro, polisi waliongozana na mtendaji na mtoto Obedi ili kupata mahali anapoishi Mzee Mapambano, zoezi hilo lilifanikiwa na mzee mapambano alikamatwa kwa ajili ya kuhukumiwa kwa tuhuma zinazomkabiri.

Ukweli ni kwamba kuhukumiwa kwa mzee Mapambano inaweza kuwa niadhabu kwa mzee huyo lakini isiwe suruhisho kamili kwa watoto walioathirika na ukatili huo. Kulea watoto sio tu kuhakikisha mtoto anakula, anavaa, analala na anasoma lakini pia ni pamoja na kuhakikisa mtoto anakuwa na afya njema ya kiakili na mwili, mtoto aweze kuwa na uwezo wa kuelezea matatizo anayokutana nao katika ratiba yake ya kila siku. Hivyo wazazi, walezi, walimu na jamii nzima lazima washirikiane katika kumlinda mtoto na sio kusubiri tatizo kutokea ili wamhukumu mtuhumiwa.