• +123-456-7890
  • info@example.com
  • Tyagal, Patan, Lalitpur
Uncategorized
CASE STORY UNYANYASI WA MTOTO WA KIKE

CASE STORY UNYANYASI WA MTOTO WA KIKE

Majina yaliyotumika katika kisa hiki ni ya kubuni, ili kuficha usiri wa walengwa.
Familia moja iliyokua na mzazi mmoja ambae ni baba (mzee Kavuma miaka 56) na mabinti
wawili, mmoja alikuwa ni mtoto wake aliezaa na marehemu mke wake aliefahamika kwa jina la
Nzela (jina la kubuni13) na mwingine alikua mtoto wa marehemu dada yake (mpwa wake)
aliefahamika kwa jina la Dallah (jina la kubuni 13). Mabinti wote walikuwa niwanafunzi wa
kidato cha kwanza katika shule ya selikari iliyokuwa mbali kidogo na nyumbani. Mzee Kavuma
alikua akifanya kazi ya Ulinzi, wakiendelea na Maisha ya kila siku, Nzela aligoma kwenda shule
kwa muda wa wiki moja baada ya kuulizwa alidai kuwa apewi pesa ya kula shule kama
ilivyozoeleka, lakini akaulizwa mbona mwenzio anaenda shule? Nzela hakuwa na majibu ila
alidai anataka kuhamia kwa bibi ake na akasomee huko. Baada ya siku kadhaa Nzela
alihamishiwa kwa bibi yake ambako umbali wa shule uliongezeka, lakin hata baada
kuhamishiwa huko Mzee Kavuma hakuwahi kutoa pesa ya matumizi kwa ajili ya binti yake hivyo
binti alilalamika kwa bibi ake ambae hakua na kipato na baadae kesi ilifika katika ofisi ya kata
iliyopo katika kata anayoishi Mzee Kavuma. Afisa mtendaji alimuita Mzee Kavuma kwa
mahojiano zaidi, mzee yule alidai kuwa ni kiburi cha mtoto, pia alijibu Nzela hapendi kusoma
mbona mwenzie anaenda shule na anasoma vizuri bila kulalamika, Afisa mtendaji ilibidi afanye
mahojiano ya siri na Dallah ambae alionekana binti Mtiifu kwa Mzee Kavuma ili kujua tatizo liko
wapi. Siku ya ijumaa taarifa ilimfikia Dallah shule kuwa anahitajika ofisi ya kata baada ya vipindi
na kwakuwa ijumaa vipindi vinaisha mapema binti huyo alifanikiwa kufika ofisi ya kata, aliulizwa
wewe unaishi vipi na mjomba wako, binti alielezea anaishi nyumba ya chumba kimoja na
mjomba wake, mwanzo kabla ya Nzela kuondoka yeye na Nzela walikua wakilala chini lakin
baada ya kubaki wawili mjomba wake alimwambia walale kitanda kimoja hivyo kwa sasa
wanaishi kama mke na mume. Lakin aliulizwa yeye kama hakuwahi kuacha kupewa ele ya
matumizi na mjomba wake kwa Sababu zozote zile, nae alijibu akiwa kidato cha kwanza
alipokua anakataa kuwa mpenzi wake alipigwa na kunyimwa mahitaji yote ya muhimu bila mtu
yoyote kujua lakini pia alikua anatishiwa kufukuzwa nyumbani hivyo ilibidi amkubali mjomba
wake kama mpenzi wake, aliendelea kwa kusema hata kuondoka kwa Nzela ni mpango wa
mjomba wake ili wabaki wawili waishi bila kujificha.

Pasipo kuwa na usimamizi mzuri wa malezi kwa watoto wakike, jamii itaendelea kumuona
mtoto wa kike ni dhaifu lakin Sababu kuu itabaki kuwa ni ukosekanaji wa malezi bora kwa
mtoto.

<?php if ( function_exists( ‘wpsp_display’ ) ) wpsp_display( 522 ); ?>

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *